Kamanda wa polisi aihama ofisi yake

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Kamishna Ulrich Matei ameihama ofisi yake na kuweka kambi katika vijiji vya Wilaya ya Kilosa ambavyo vimekuwa na historia na changamoto kubwa ya migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji

Kamanda Matei amefikia maamuzi hayo kupiga kambi katika vijiji hivyo ili kuhakikisha amani na utulivu vinaendelea kuwepo katika maeneo hayo ambayo katika kipindi cha kiangazi huwa na migogoro mikubwa ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji wilayani humo. 
Mbali na hilo Matei amewatia mbaroni wafugaji wanne wa jamii ya Kimasai ambao walikuwa na zaidi ya ng'ombe 800 kwa tuhuma za kulisha mifugo hiyo kwenye mashamba ya wakulima Kilosa. 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo