Walimu Wanawake Iringa walilia Usawa katika Uongozi

Walimu wanawake manispaa ya Iringa walalamikia kutokuwepo kwa uwiano wa viongozi wanawake na wanaume katika baadhi ya nafasi kama vile wakuu wa shule, maafisa elimu kata na wilaya wakati walimu wa wanawake ndio wengi hivyo inafifisha ndoto za kuwa viongozi kwa kuwa wanauwezo wa kuongoza na kusimamia mambo mengi yakaenda kama yalivyopangwa.
Hayo yamesemwa na walimu wanawake katika mkutano mkuu wa chama cha walimu wanawake kilichokuwa kinaongozwa na katibu wa wilaya mwl. Fortunata Njalale katika ukumbi wa chuo kikuu huria tawi la Iringa.
Akisoma risala iliyoandaliwa na kamati ya kitengo cha walimu wanawake MWL. Evon Mhewa alisema kuwa walimu wanawake wamekuwa wakikumbana na changamoto nyingi katika kukamilisha majukumu yao.
“Mwalimu wa kike anacheleweshewa kulipwa madeni mbalimbali anayokuwa anaidai serikali maana bila kulipwa madeni yetu walimu hawawezi kufundisha kwa moyo kwa kuwa maisha yanakuwa magumu na kuwapelekea kubuni njia mbadala za kujiingizia kipato,” alisema Mhewa
Mhewa alizitaja changamoto nyingine ni kutopata nyongeza ya mishahara ya kila mwaka na kusimama kwa mwaka wa pili sasa,walimu kutopandishwa madaraja na wengine kupandishwa na kupokwa mshahara pamoja na walimu wanawake kutokuwa na uwiano wa vyote katika sekta nyeti.
“Sisi walimu wa kike kwa sasa tumesoma sana na tunaweza kuwa viongozi sehemu yoyote kwa kuwa tayari tumethibisha hilo kwa wanawake waliopewa kazi hiyo kwani wameifanya ipavyo na kuleta matokeo chanya kwa serikali hivyo tunaomba walimu wanawake tupewa nafasi katika ngazi ambazo tunastahili” alisema Mhewa.
Akijibu risala hiyo mgeni rasmi ambaye ni afisa elimu manispaa ya Iringa MWL .Tupe Kayinga alisema kuwa ni kweli walimu wanamadi mengi serikalini lakini akasema kuwa hiyo yote imetokana na swala la uhakiki wa watumishi hivyo mchakato wa uhakiki ukimalizika kila kitu kitakuwa sawa ninauhakika na hilo.
“Unajua serikali imechelewesha maswala mbalimbali ambayo ni kero kwa walimu kutokana na uhakiki hivyo nawaomba walimu wawe na uvumilivu kwa kuwa kila kitu kitakuja kutengemaa kama ilivyokuwa hapo awali”alisema Kayinga
Kayinga aliwataka walimu wanawake kuendelea kusoma ili kuwa na elimu ndio itakayowapa nafasi mbalimbali ambazo zinashikiriwa na walimu wanaume hivyo bila kuwa na elimu walimu wanawake wataendelea kuongozwa na walimu wanaume kila sekta.
“Najua kuwa walimu wanawake wanakipawa cha kuwa viongozi lakini mitaala mingi inataka walimu kuwa na elimu ili kupata kuongoza sekta mbalimbali sasa inatubidi walimu kujiendeleza kimasomo ili kukidhivigezo ambavyo mara nyingi imekuwa ni elimu ya walimu anayepaswa kupewa kitendo husika” alisema Kayinga
Aidha Kainga aliwataka walimu wanawake kugombea nafasi mbalimbali zinazojitokeza ili kupata nafasi za kuongoza na sio kila wakati kuwaacha walimu wanaume wakigombea pekee yao.
“Tumieni fursa za kugombea nafasi zinazojitokeza msiogope wanawake mnatakiwa kuwa mstari wa mbele kuogmbea kwa kuwa katika kada ya ualimu walimu wanawake tupo wengi hivyo kuanzia saizi walimu wanawake amkeni mjitume kuhakikisha mnagombea” alisema Kayinga
Naye katibu wa chama cha walimu wilaya ya Iringa mwl. Fortunata Njalale alisema kuwa mkutano huo ni wa kikatiba kwa mjibu wa katiba ya chama cha walimu taifa hivyo katiba imewaagiza kukaa na viongozi wa walimu wanawake kuzijadili changamoto za wanawake ili kuzipeleka katika mkutano mkuu wa wilaya.
“Leo tupo walimu wanawake pekee yetu ili kubaini changamoto zetu na kuzipeleka kwenye mkutano mkuu na kuweza kuzitetea kwa pamoja ili kuboresha maslai ya walimu wanawake ambao wamekuwa wanakumbana na changamoto nyingi sana wawapo kazini” alisema  Njalale
Njalale alisema kuwa walimu wanawake wamekuwa na mwamko wa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kuwa wanauwezo wa kuwa viongozi na kuongoza kwa kupata matokeo chanya.
“Tunakitengo cha walimu wanawake taifa kimetusaidia sana walimu wanawake kupata ujalisi na kuacha uoga kugombea nafasi mbalimbali hivyo kwa sasa walimu wakiume wajipange sana maana walimu wanawake tumedhamilia kugombea nafasi yeyeto itakayojitokeza katika chama chetu cha walimu” alisema Njalale
Njalale aliwapongeza walimu wanawake wanaothubutu kugombea nafasi mbalimbali kwa kuwa wamekuwa wakishinda na wanafanya kazi ipasavyo na kusema kuwa walimu wanawake wanaweza bila kuwezeshwa.
Na Fredy Mgunda, Iringa


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo