Rai imetolewa kwa wafanyabiashara wilayani Makete mkoani
Njombe kutunza kumbukumbu za biashara zikiwemo za manunuzi ili kutoleta
mkanganyiko wa kiasi cha kodi anachostahili kulipa mfanyabiara wakati wa
ulipaji wa kodi
Akitoa elimu kwa mlipa kodi kwa wananchi wa Tandala na
maeneo ya jirani katika semina iliyofanyika katika ukumbi wa MTC Tandala yenye lengo la kuongeza mapato ya serikali na
kupitia mabadiliko ya sheria ya kodi kwenye bajeti ya serikali kwa mwaka wa
fedha 2017/2018, afisa elimu na huduma
kwa mlipa kodi kutoka mamlaka ya mapato Tanzania TRA Kefa Mwambene
amesema ni vema wafanyabiashara wakatunza kumbukumbu za biashara zao ili kutoleta
mikanganyiko baina ya maafisa wa TRA na wafanyabiashara wakati wa ulipaji kodi
Awali wafanyabiashara walipata nafasi ya kuuliza maswali
na kutoa mapendekezo ya namna bora ya ukusanyaji wa mapato na kujenga uhusiano
baina ya TRA na wateja wake huku wakieleza adha wanayoipata wakati wa operesheni
mbalimbali zinazofanywa na mamlaka hiyo kupitia wakala wake kampuni ya YONNO
ACTION MART na baadaye afisa wa TRA akatolea ufafanuzi
Green fm imefanya mahojiano na wafanyabiashara Nje ya
ukumbi mara baada ya kumalizika kwa semina hiyo na kuelezea jinsi semina hiyo
ilivyowasaidia kutambua mambo mbalimbali
ikiwemo majukumu na haki ya mlipa kodi
Katika mwaka wa fedha 2017/2018 serikali imepanga
kukusanya kiasi cha shilingi trilioni 31.7
kupitia vyanzo vya mapato mbalimbali ambapo mamlaka hiyo ya mapato Tanzania pekee imepanga kukusanya
shilingi trilioni 17 katika bajeti hiyo
Na Riziki Manfred