Mwalimu Gregory Emmanuel
Mwalimu Thobis Kasambala
Wakati Oktoba 5 ya kila mwaka Dunia huadhimisha siku ya
walimu, baadhi ya walimu wilayani Makete mkoani Njombe wameonesha kufurahia wao
kuwa walimu huku wengine wakiiomba serikali kuwalipa madai yao
Wakizungumza na Green FM walimu hao Wakiwemo Tobisa
Kasambala, Gregory Emannuel na Mchungaji Luka Lwila wamesema walimu ni nguzo
muhimu katika jamii ambayo imesaidia kuielimisha jamii kwa kuwa kila mtu kwa
nafasi yake amepitia mikononi mwa walimu bila kujali ni mwalimu wa mfumo rasmi
ama asiye wa mfumo rasmi
Miongoni mwa walimu hao Bw. Thobias Kasambala amesema
anaipongeza serikali ya awamu ya 5 katika kutekeleza baadhi ya mambo ikiwemo
kuondoa watumishi hewa ambapo na walimu wameguswa na wao kama walimu wanaunga
mkono uamuzi huo wa serikali
Siku ya walimu duniani
imekuwa ikiadhimishwa kila mwaka ifikapo oktoba 5 na mtandao wa
elimu Tanzania TENMET, lakini hapa
nchini imekuwa ikiadhimishwa kila baada ya miaka 3, Na hatua hiyo imekuja baada
ya makubaliano yaliyofanyika mjini paris mwaka 1966 baina ya shirika la elimu na utamaduni duniani UNESCO na shirika la kazi duniani
ILO.
Sikiliza sauti zao kwa kubonyeza Play hapo chini:-