Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli amesema kutokana na matendo maovu yaliyokuwa yanaendelea serikalini, nchi ilikuwa inaelekea kuzimu
Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati akifungua mkutano wa 33 wa jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania jijini Dar Es Salaam ambapo amesema miongoni mwa vitu vilivyokuwa vinafilisi nchi ni watumishi hewa na wenye vyeti hewa
Rais amesema "Kwa sasa kero hiyo imeondoka baada ya kudhibiti na kuwaondoa watumishi hewa na wale waliokuwa na vyeti hewa, unakuta mtu ni kilaza hajasomea anachokifanyia kazi, wewe uliyesomea mnajikuta mnalipwa mshahara mmoja, hii ilikuwa inaumiza sana, lakini sasa nidhamu imerejea"
#MKUTANOALAT "Nimeagiza shilingi bilioni 38 zilizokuwa zikilipa pensheni hewa zirudishwe Serikalini"-Rais @MagufuliJP— Msemaji wa Serikali (@TZ_MsemajiMkuu) October 3, 2017
Rais Magufuli: Ndio maana elimu ilikuwa inadharaulika kwani watu walikuwa wanajipatia mishahara mikubwa kwa vyeti vya kutengenezwa#JFLeo— Jamii Forums (@JamiiForums) October 3, 2017
