Mambosasa amesema kuelekea mchezo huo wa watani wa jadi hapo kesho jeshi la polisi limejipanga na kuimalisha ulinzi ambapo amedai kwa mara ya kwanza atatumia magari ambayo yamefanyiwa ukarabati na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ili kuboresha ulinzi katika mchezo huo.
"Uwanja utafunguliwa kuanzia saa mbili na nusu asubuhi yoyote ambaye atataka kuangalia ile mechi awahi mapema, uwanja ukishajaa hatutaruhusu watu kuingia na ulinzi umeimarishwa kutakuwa na askari watakaokuwa doria za miguu, pikipiki, mbwa. farasi na kwa mara ya kwanza nitatumia magari yaliyotengenezwa na Mhe. Makonda kesho yataingia pale uwanjani yakiwa yamesheheni askari ambao watakuwa timamu kwa ulinzi kukabiliana na jambo lolote" alisema Mambosasa
Aidha Kamanda Mambosasa aliendelea kufafanua kuwa "Nitoe onyo kwa mashabiki ambao si wastaraabu mashabiki ambao wanakwenda pale lakini hawataki matokeo ya ndani ya dakika 90, ni bora mtu abaki nje au akaangalie kwenye Luninga ila yoyote ambaye atakuja Uwanja wa Uhuru ninawataka wafuate sheria, watulie washangilie wasifanye uhalifu wowote hatutakubali wala kumvumilia mtu yoyote atakaefanya uharibifu wa kung'oa kiti, kurusha jiwe, au kufanya kitu chochote ambacho sicho na niwaambie tu wote wakati wa kuingia tutawakagua" alisisitiza Mambosasa.