Lazaro Mambosasa amesema hayo leo alipokuwa akilaani kitendo cha mauaji dhidi ya polisi huyo wa kikosi cha kutuliza ghasia ambaye aliuwawa na watu wasiojulikana na kisha mwili wake kutupwa kwenye uzio wa kambi ya FFU Ukonga.
"Mnamo tarehe 21 majira ya saa sita za usiku yalitokea mauaji maeneo ya kambi ya polisi Kikosi Cha Kutuliza Ghasia (FFU) Ukonga Makao Makuu, ilipofika alfajiri mwili wa askari PC Charles Yanga uliokotwa ukiwa pembeni mwa uzio wa kambi hiyo ya Ukonga ukiwa umeangushwa chini, huku pikipiki yake ikiendelea kuwasha taa za 'hazard' mwili ilipochunguzwa majeraha yalionekana kwenye paji la uso la huyo kijana lakini pia sikio moja lilikuwa limekatwa kabisa na kuondolewa. Katika ufuatiliaji wa polisi walibaini kuwa polisi huyo ameuwawa na watu ambao bado tunawafuatilia na hatujafanikiwa kuwatia mbaroni bado" alisema Mambosasa
Kamanda Mambosasa amesema kuwa watuhumiwa hao wakikamatwa watafikishwa kwenye vyombo vya dola kwa hatua za kisheria