Kwenye ukurasa wake wa twitter Joshua Nasari ameandika ujumbe huo, akisema kwamba kuna haja ya Zitto Kabwe kufanya hivyo kwani wakati uliopo sio salama tena.
"Nadhani ni wakati sahihi sasa ndugu yangu Zitto Kabwe ukaongeza ulinzi wako binafsi, nyakati hizi si salama tena kama tudhaniavyo", ameandika Joshua Nasari.
Hivi karibuni baadhi ya wabunge wa upinzani wameripoti kuhofia usalama wao, kwa kufuatiliwa na watu wasiojulikana na kutishia maisha yao.
Alichokiandika Joshua Nasari twitter