PICHA; Miili ya Marehemu waliokufa Ziwa Victoria kwenye ajali ya Hiace

Watu wanane wamekufa na wengine wameokolewa wakiwa salama baada ya Toyota Hiace kutumbukia Ziwa Victoria katika kivuko cha Kigongo Feri wilayani Misungwi.

“Kwa sasa uokoaji unaendelea, abiria kadhaa  ndio wametoka salama. Maiti nane zimeopolewa,” amesema Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa) Mkoa wa Mwanza, Ferdinand Mshama.Temesa ndiyo inasimamia kivuko hicho.

Mshama amesema gari hilo linafanya safari kati ya Buhongwa jijini Mwanza na kivukoni hapo.

Amesema ajali hiyo imetokea kutokana na gari hilo kupata hitilafu kwenye mfumo wa breki hivyo liligonga geti la kivuko na kutumbukia ziwani.

“Ni kweli gari limetumbukia, lilikuwa likitokea Buhongwa kupeleka abiria kivukoni, kabla dereva hajapaki lilifeli breki,” amesema na kwamba dereva alipita upande wa magari makubwa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo