Basi la Kampuni ya Japanese aina ya Mitsubishi Rosa lenye namba za usajili T437 CLT limepata ajali baada ya kufeli breki eneo la mpaka wa kijiji cha Luvulunge na Iwawa Makete
Ajali hiyo imetokea leo mchana majira ya saa 7 likiwa limetokea Mbeya kuelekea Ikonda wilayani Makete ambapo zaidi ya abiria 20 waliokuwa ndani ya basi hilo wamepata majeraha madogomadogo katika miili yao na wanapata matibabu Hospitali ya Wilaya Makete huku wengine wakiruhusiwa kurudi makwao
Chanzo cha ajali hiyo kwa Mujibu wa Dereva Noah Sanga amesema ni kufeli kwa breki za basi hilo likiwa Kwenye mteremko mkali na kuacha barabara likaelekea mtoni na kuvuka mto huo kisha likasimama kama picha zinavyoonesha
Majeruhi wakiendelea kutibiwa





