Mjane amwaga Machozi Mbele ya Rais Magufuli

Rais John Magufuli amewaaigiza Mkurugenzi Jiji la Mwanza, Mkuu wa Mkoa, John Mongella na Naibu Waziri wa Ardhi, Angelina mabula kuhakikisha wanashughulikia na kutatua suala la mjane Anna Joyce Francis mkazi wa Isamilo wilayani Ilemela anayedai kudhurumiwa ardhi na mtu aliyemtaja kuwa ni mwanasheria.

Hayo yamejiri leo jijini Mwanza wakati Rais Magufuli akiwahutubia wananchi wa mkoani humo ambako amefanya ziara ya siku mbili kuzindua miundombinu mbalimbali.

“Mhe. Rais mimi ni mjane, nimedhurumiwa ardhi yangu na mwanasheria anaitwa Alex Bandulaki,niliinunua kwa mzawa lakini amekuja anasema aliuziwa na Jiji. Miaka tisa nahangaika amenipeleka mahamani, wanangu wameteseka.

“Barua zangu zimefishwa mahakama ya wilaya anaambiwa ameshinda kesi, hukumu yenyewe ikitoka yake imeandikwa tarehe nyingine na yangu imeandikwa tarehe nyingine,” Mama huyo alilalama huku akimwaga machozi mbele ya Rais.

Baada ya maelezo hayo, Rais alitoa agizo kwa viongozi hao kulishughulikia suala hilo haraka iwezekanavyo ili mama huyo aweze kupata haki yake. Aidha Rais amempa mama huyo kiasi cha fedha kwa ajili ya kujikimu.

Kwa upande mwingine Rais Magufuli amewataka Meya wa Jiji la Mwanza, James Bwire na viongozi wenguine wa mkoa huo wamalize malumbano yao ili wawatumikie wananchi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo