Mbunge Lema atapoteza muda wake - Gambo

Mrisho Gambo amefunguka na kusema Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema anapaswa kutambua kuwa yeye kama Mkuu wa mkoa anajishughulisha na matatizo ya watu hivyo kama hatabadili aina ya siasa azifanyazo  basi anapoteza muda wake kwa miaka mitano yote

Gambo amesema kuwa yeye hana tatizo lolote na Mbunge huyo wa Arusha mjini na kudai kwamba anapaswa kutambua na kubadili aina ya siasa anazofanya kwa kuwa yeye amelenga kutatua matatizo na changamoto za watu wa Arusha Mjini. 
"Msuguano na Mbunge haupo lakini anatakiwa tu asome alama za nyakati kwamba Mkuu wa Mkoa wa sasa amedhamiria kuhangaika na shida za watu kama hatalitambua hilo atapoteza muda wake kwa miaka yake yote mitano" alisema Mrisho Gambo 
Aidha Mkuu wa Mkoa huyo amesema kuwa yeye kama kiongozi kijana anahitaji zaidi kukosolewa kuliko kusifiwa ili aweze kujirekebisha sehemu ambayo ana mapungufu ili aweze kuwa kiongozi madhubuti na mahiri zaidi. 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo