Maswali Kibao ya CHADEMA Hii leo

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimehoji maswali kibao kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba na Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP), Simon Sirro,  kuhusu mambo yanayoendelea kwenye upelelezi wa kupotea kwa Ben Saanane, kushambuliwa kwa Tundu Lissu na kuhusu mtu aliyemtishia kwa bastola Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye.

Katika mkutano na waandishi wa habari leo Ijumaa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema amesema:

“Ni siku 695 tangu Mawazo (Alphonce) auawe, siku 326 tangu Ben Saanane apotezwe na watu wasiojulikana na leo ni siku 26 tangu Lissu afanyiwe jaribio la kumuua na mpaka sasa polisi hawajasema lolote, zaidi ya Nissan nane ambazoa zimehifadhiwa kusikojulikana.

“Leo tunapozungumza, viongozi mbalimbali wanaendelea kutishwa, Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya,  anatishwa na watu wamemfuata nyumbani kwake, Josua Nassari ametishwa, Lema (Godbless) ametishwa.  Ben Saanane alitishwa na alitoa taarifa Kituo cha Polisi Tabata na kapotea, Lissu alitoa taarifa kwamba anatafutwa na yaliyotokea mnajua.  Hofu ni kubwa, maiti zaidi ya 17 zimeokotwa Coco Beach hakuna ‘seriousness’ kwa matukio.

Naye Mkurugenzi wa Mafunzo na Operesheni wa Chadema, Kigaila Benson,  amesema:
“Haya mambo si ya kawaida, yanafanywa na watu wasio wa kawaida, niseme tu hakuna aliye salama, hujui kesho yako.  Kuna kijana anaandika mambo ya ajabu, kwa nini polisi hawaoni, IGP anachagua mambo ya kusikia, kwa nini ukimkosoa Rais jioni yake unakamatwa?

“Wanasema wamekamata Nissan, hivi hizi Nissan zilikuwa wapi, zilikuwa zinaendeshwa na nani?  Waziri Mwigulu anasema gari alilolitaja Lissu liko Arusha, waziri ametumia kigezo au kifaa gani kubaini gari halikuwahi kufika Dar? Kwa nini chombo hicho kisitumike kuwabaini waliomshambulia Lissu?”

“Mwigulu kwa nini amechukua uwakili wa mtuhumiwa? Amehojiana vipi na huyo? Kwa nini mtu huyo anayetuhumiwa asikamatwe na sasa anafanya kazi ya kumtetea?  Polisi wanatakiwa kutuambia, upo wapi usalama wa raia.  Tumesimama upepelezi wa tukio la Lissu kwa sababu ya dereva, ina maana kama dereva angekufa upepelezi usingekuwapo?

“Sisi hatuwezi kumficha dereva, anapata matibabu, ila kama wamesema wanafahamu gari lile lipo Arusha wanashindwaje kwenda kuzungumza na dereva?  Sirro analitumia jeshi kisiasa.   Sirro kwa nini asimuulize RPC Kaganda (Suzan) aliyekuwa Kinondoni ambaye alikuwapo siku Nape anatolewa bastola?  Kwa nini hawakumkamata?

“Jeshi la polisi ni letu sote, tusilitumie kisiasa, tunataka tueleweke kwamba IGP wanamjua huyu mtu.  Kwa nini wanamtafuta mtu ambaye walikuwa naye, hivi kwa nini maswali magumu wanakuwa na majibu ila maswali mepesi wanakosa majibu?”


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo