Mahabusu walipiga kelele kuniokoa Nisifie Mahabusu – Ester Bulaya

Mbunge wa Bunda mjini kupitia CHADEMA, Ester Amos Bulaya, kwa mara ya kwanza ameelezea kile kilichojiri akiwa mahabusu mpaka kupelekea kupoteza fahamu na kulazwa

Akizungumza na mwandishi wa habari wa East Africa Television, Ester Bulaya amesema sababu ya kukamatwa kwake ilikuwa kwa kosa la kwenda kutoa misaada kwenye shule iliyopo kwenye jimbo la mbunge mwenzake wa CHADEMA John Heche.
Ester Bulaya ameendelea kusimulia kwamba baada ya kumkamata akawaambia kwamba ana tatizo la pumu, hivyo wasimuweke kwenye mazingira ambayo yanaweza yakamletea matatizo kiafya, lakini wakamuingiza mahabusu bila kujali afya yake, na baada ya muda hali ikaanza kubadilika, na ndipo mahabusu wenzake aliokuwa nao ndani wakaanza kupiga kelele wakiwa ndani ili polisi waje wasaidie.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo