Katibu mwenezi wa CCM ahamia CHADEMA

Aliyekuwa Katibu  Mwenezi wa CCM Wilaya ya Nyasa, Staniford Emmanuel amehamia Chadema kwa maelezo kuwa wakati wa ukombozi umefika.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi kadi hiyo kwa viongozi wa Chadema, Emmanuel amesema wakati wa ukombozi umefika hivyo hana budi kuhama CCM ili aweze kutendea haki nchi yake.

“Kuna wanaCCM wenzangu bado hawajafanya maamuzi kama niliyoyafanya mimi kujiondoa na kuhamia chama cha ukombozi ambacho mimi nimekiona ni Chadema,”amesema Emmanuel.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo