Mtu mmoja amefariki kwa ajali ya moto akiwa katika jitihada za kuokoa miti yake iliyokuwa ikiteketea kwa moto uliowaka kwa muda wa siku nne mfululizo katika kijiji cha Ugabwa kilichopo kata ya Lupalilo Makete
Marehemu huyo aliyetambulika kwa jina la Baraka Sanga (58) aliondoka nyumbani kwake juzi jumapili akiwa peke yake baada ya kuona moto unateketeza miti ndipo alipoelekea shambani ili kuzuia moto huo usiteketeze miti ya mbao aliyopanda
Akiwa huko alizidiwa na moto huo mpaka kusababisha kifo chake na mwili wake umekutwa Leo ukiwa umeungua vibaya
Taarifa hii ni kwa mujibu wa ukurasa wa facebook wa Kituo cha Redio Kitulo FM Makete