Nape Nnauye amedai kuwa Uhuru Kenyatta anastahili kuwa Rais wa Kenya kwa sababu yeye ni mwana demokrasia wa kweli hivyo anaamini raia wa Kenya watampa kura nyingi za kutosha na kumpuuza mpinzani wake Raila Odinga.
"Unastahili kuwa Rais wa Kenya. Mwana demokrasia wa kweli. Naamini ndugu zangu wa Kenya watakuchagua kwa kishindo kesho na kumpuuza kibaraka" ameaandika Nape Nnauye kupitia mtandao wake wa twitter.
Nchi ya Kenya kesho inategemewa kufanya uchaguzi wa marudio wa nafasi ya urais kufuatia mahakama ya juu nchi humo kufuta matokeo ya urais.