Aliyemshika makalio mwanaume mwenzake kutupwa jela miaka mitatu

Mwanamme mmoja raia wa Uingereza huenda akatupwa jela miaka mitatu kwa kosa la kumshika mwanaume mwenzake makalio wakiwa Bar jijini Dubai.
Jamie Harron
Jamie Harron (27) ambaye alienda kutalii Dubai alikuwa kwenye Bar moja iitwayo Rock Bottom Bar ambapo baada ya kulewa hadharani alijikuta akimtomasa sehemu za makalio mwanaume mwenzie aliyepita karibu na meza yake.
Wahudumu walioshuhudia tukio hilo  walitoa taarifa polisi na dakika 20 baadae Bw. Harron alidakwa na maaskari polisi na kuswekwa rumande.
Polisi mjini Dubai wamesema kuwa walimshikilia Bw. Harron mwezi Julai mwaka huu kwa makosa ya kunywa pombe kupitiliza na kuonesha ishara ya vitendo vya kishoga na baadae siku tano alifikishwa mahakamani.
Taarifa za kukamatwa kwake zilikuwa na usiri mkubwa kabla ya vyombo vya habari vya kimataifa kutangaza tukio hilo.
Hata hivyo kesi yake ilipangwa kusikilizwa mara tatu lakini mtuhumiwa hakufika mahakamani.
Harron amesema mpaka sasa passport yake na nyaraka zake muhimu zimekamatwa na mpaka sasa ametumia dola $30,000 kujikimu.
Tayari passport ya Harron imeshakamatwa na serikali na Oktoba 30 mwaka huu atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo zinazomkabili.
Tayari wanaharakati mitandaoni wameanza kuishambulia bodi ya utalii Dubai kwa kudai kitendo hicho ni cha uonevu na kitawapunguzia idadi ya watalii.
Kwa sheria za Falme za Kiarabu Bwana Harron kwa kosa la kunywa pombe hadharani atahukumiwa miezi mitatu jela au kupigwa faini, na kama atapatikana na hatia kwenye tukio la kumshika mwanaume mwenzake makalio basi atafungwa miaka mitatu jela. Vifungu vya sheria hiyo ni kwa wageni tu na watu ambao sio waislamu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo