Mbunge huyo ametoa vifaa na vyakula hivyo, kwa ajili ya wanafunzi hao ambao wataanza mtihani wa taifa wa kidato cha nne mwaka huu siku ya kesho Oktoba 30.
Mh. Ungando ametoa vitu hiyvo kama sehemu ya kutimiza ahadi yake kwa shule zote za sekondari za jimbo la Kibiti. Utaratibu huo wa kutoa mboga na vyakula ulianza mwaka jana ambapo mbunge huyo alifanya hivyo kwa shule zote.
Aidha Ungando ameahidi kuendelea kutatua na kusimamia kero mbalimbali zinazozikabili sekta za elimu, afya, miundombinu na masuala ya kijamii ikiwemo kuwezesha makundi maalum.