Mwanaume huyo aliyejulikana kwa jina la Valentino Talluto mwenye umri wa miaka 33, alikuwa akiwashawishi wanawake hao kufanya nao ngono bila kujikinga, kwa madai kwamba amepima karibuni na ana 'allerg' na condom.
Valentino alikuwa akiwapta wanawake hao kwa kutumia mitandao ya kijamii na kuwarubuni, huku akiwa na mahusiano na wanawake zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja.
Waendesha mashtaka wa mjini Roma Italia, waliomba apewe kifungo cha maisha jela, lakini baada ya majadiliano ya masaa 12 mahakama iliamua kumfunga miaka 24 jela.
Akiwa mahakamani Talluto alielezea kujuta kwake kwa kufanya kitendo hicho, na kusema kwamba hakujua madhara ya vitendo hivyo.
Wanawawake wengi walikutwa na HIV kutokana na matatizo ya kiafya baada ya kufahamu juu kukamatwa kwa Talluto, na miongoni mwa wanawake hao mmoja ni binti aliyekuwa na miaka 14.
DW