Zungu: Watoto wenyewe wana wajibu wa Kuzuia Mimba

Mwenyekiti wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Azzan Zungu amesema hakuna sheria yoyote itakayo tungwa na bunge kuzuia mimba za utotoni hapa nchini, isipokuwa watoto wenyewe ndio wanaowajibika kufanya hivyo

Azan Zungu ameyasema hayo katika hafla ya 15 ya kuhitimu elimu ya sekondari katika shule ya sekondari ya wasichana ya Babro Johansson ya jijini Dar es salaam.
"Niwasihi hakuna sheria yoyote itakayofungwa na bunge itakayozuia mimba za utotoni, hakuna sheria iitakayozuia mimba mashuleni, mimba zitazuiwa na nyinyi pamoja na wazazi wenu na jamii kiujumla", amesema  Azan Zungu.
Azan Zungu ameendelea kwa kuwataka wanafunzi wengine kujitunza ili kuweza kuhitimu elimu yao salama, na kuja kujikomboa hapo baadaye na kujenga taifa lenye wasomi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo