Amchinja Mkewe na yeye Kujiua Kinyama Pia

Watu wawili mume na mke wamefariki dunia katika kijiji cha Mwagiligili mkoani Mwanza baada ya mume Kwilokeja Boniphace (35) kumuuwa mkewe Shija Luchagula (30) kwa kumpiga na kumnyonga kisha yeye kujinyonga kwa kile kinachosemekana ni wivu wa mapenzi

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mtuhumiwa wa mauaji hayo alikuwa akimtuhumu mkewe kuwa anatoka kimapenzi nje ya ndoa hali iliyopelekea ugomvi kati yao.
"Inasemekana kuwa mtuhumiwa wa mauaji hayo alikuwa akimtuhumu mkewe kuwa anatoka nje ya ndoa hali iliyopelekea kuzuka kwa ugomvi wa mara kwa mara baina yao. Inadaiwa kuwa kabla ya tukio hilo la mauaji kutokea siku hiyo mtuhumiwa aliamka asubuhi na kufagia uwanja wa nyumba yao kama mtego wa kubaini watu wanaokuja hapo nyumbani kwake, kisha alikwenda kwenye shughuli zake za kawaida" Ilisema taarifa ya Msangi 
Kamanda Msangi aliendelea kusema kuwa 
"Inadaiwa kuwa baada ya muda mchache kupita mtuhumiwa alirudi nyumbani, ndipo akiwa hapo nyumbani kwake aliona matairi ya baiskeli katika uwanja wa nyumba yake ndipo ulizuka ugomvi kati yake na mkewe huku akimtuhumu mkewe kuwa alikuwa si mwaminifu katika ndoa hapo nyumbani kwake na kupelekea kumpiga mkewe hadi kumuua na yeye mwenyewe kujinyonga hadi kufa" 
Miili ya wanandoa hao imekabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi. 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo