Yanga yaipigia magoti bodi ya Ligi

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga kupitia Kaimu Afisa Habari wao Godlisten Anderson 'Chicharito' wameiomba bodi ya Ligi kukahikisha ratiba inaendelea kubaki kama ilivyo ili isije kuwaumiza wachezaji kisaikolojia.

Chicharito ameeleza leo ikiwa zimebakia siku chache kuelekea mchezo wao wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaopigwa Septemba 10 katika uwanja wa Sabasaba mjini Njombe na kusema hawawezi kubishana na wapanga ratiba ila wanavyokuwa wanabadilisha mara kwa mara wanawatoa wachezaji katika molali ya mchezo.

"Kikawaida hatuwezi kubisha kwa sababu ratiba imeshatoka kikubwa ni kuifuata kama ilivyopangwa lakini tunawaomba wapangaji wa ratiba wajitahidi iendelee kubakia kama ilivyo isiwe na mabadiliko ya kila mara", amesema Chicharito.

Pamoja na hayo, Chicharito amesema mpaka hivi sasa wachezaji wake wote wanaendelea na mazoezi ya kujiandaa na mchezo huo dhidi ya Njombe Mji FC.

"Kikosi bado kinaendelea na mazoezi yake katika uwanja wa Uhuru, kuhusu suala la safari tutatoa taarifa maalumu kwamba itakuwa siku gani kwa sababu tumeambiwa mechi itakuwa siku ya Jumapili", amesisitiza Chicharito.

Kwa upande mwingine, Chicharito amesema kwa mujibu wa taarifa alizozipokea kwa daktari wa timu hiyo kuwa wachezaji majeruhi wameshaanza mazoezi mepesi ya kuweka mwili sawa kuanzia siku ya jana ili waweze kujiunga na wawenzao.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo