Naibu Waziri amefikia uamuzi huo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani, Tumbi Septemba 27 mwaka huu na kubaini kusimama kwa mradi huo kwa muda mrefu.
Akizungumza na watumishi wa Hospitali hiyo pamoja na viongozi wa Mkoa Naibu Waziri Jafo ameeleza kusikitishwa na namna ambavyo mradi huo umetelekezwa kwa miaka saba hali ambayo imesababisha majengo kuchakaa kabla hata ya kuanza kutumika.
“Natoa wiki moja kwa Mtendaji mkuu kufanya haraka iwezekanavyo ujenzi wa mradi huu wa upanuzi ambao ulikuwa umesimama kwa kipindi kirefu uanze mara moja maana fedha zipo na tumeshazitoa shilingi milioni 600 sasa sijui nini tatizo kwa hiyo wiki ijayo nataka kuona ujenzi huo unaanza kuendelea”, amesema Jafo.
Aidha Waziri Jafo alipata fursa ya kusalimiana na wagonjwa waliolazwa Hospitalini hapo kwaajili ya kupata huduma za afya.