Hayo yameelezwa mbele ya Mahakama ya mwanzo ya kata ya Makorongoni Manispaa ya Iringa baada ya kupita takribani siku tatu tokea mbunge huyo kuachiwa kwa dhamana ya Polisi.
Mchungaji Peter Msigwa alikamatwa na Jeshi la Polisi septemba 24, mwaka huu wakati yupo mkoani humo akihutubia wananchi katika mkutano wa wazi uliyofanyika katika kata ya Mlandege na kuachiwa kwa dhamana ya watu wawili ambao ni Alex Kimbe pamoja na Mwenyekiti wa Bavicha Iringa Leonce Marto saa nne usiku wa siku hiyo hiyo.
