Na Mahmoud Ahmad Arusha
Chama cha Mpinduzi wilayani hapa kimepokea wanachama wapya zaidi ya 300 kutoka vyama mbali mbali vya upinzani na kuzindua mashina matatu ya wakereketwa katika kata ya Levolosi jijini hapa.
Akiwapokea wanachama hao wapya waliorudi kundi katika ukumbi wa chama hicho mkoani hapa Katibu wa ccm mkoani hapa Elias Mpanda alisema kuwa chama hicho kinachongoza serikali kimejipanga kuhakikisha kinarudisha misingi imara iliyoasisiwa na Mwalimu Nyerere ya kuwajali wanyonge bila kujali itikadi zao kisiasa,kidini wala Rangi nah ii imewafanya wananchi kurudisha imani kwa chama hicho.
Amesema kuwa Serikali inayoongozwa na mwenyekiti wa chama hicho imekuwa ikihakikisha inashughulika na kero mbali mbali zinazowagusa wananchi wa hali za chini nah ii imeongeza kuwasogeza wale waliokuwa wameondoka na kukimbilia upinzani kuona sasa kero zao zimepata mtu sahihi wa kuzishughulikia.
“ Umeona misingi ya chama imeanza kufanyakazi na Arusha mpya inazaliwa upya lengo likiwa ni kurudisha chama kwa wananchi na si wachache hichi ni chama chao kimsingi wananchi wanao fursa nzuri ya kujiunga wakati wowte kama hawa”alisema mpanda.
Wanachama hawa wapya watambea misingi yao kama wanachama ikiwemo kuhakikisha kuwa mabalozi wazuri wa kukihubiri chama kuanzia ngazi ya matawi hadi mkoa ili kukijenga chama ndani ya mkoa wetu.
Kwa upande wake Katibu mwenezi mkoani hapa Shaban Mdoe alisema kuwa ccm imewapokea wanachama hao zaidi ya mia tatu kutoka vyma vya upinzani nakuahidi kuwa chama hicho mkoani hapa kimejipangakwa lengo mmoja la kuhakikisha wanarudi nyuma kuwatumikia wananchi wanyonge chini ya serikali ya Rais dkta Magufuri.
Mdoe alisema kuwa wanachama wapya wanaopokelewa leo wawe mabalozi wazuri wa kukitangaza chama kuweza kuendelea kushika dola kwani msingi wa chama ni wanachama na wao wameweza kuwarudisha kundini wanachama hao waliokimbilia upinzani.