Mwigulu: Uchunguzi wa Lissu kushambuliwa unaendelea, tutatoa taarifa

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, amesema gari ndogo ambayo Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, alidai lilikuwa likimfuatilia maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam, iko Arusha na haijawahi kutumika Dar es Salaam.

Mwigulu amesema leo kuwa baada ya polisi kufuatilia gari hiyo wamegundua iliyokuwa inamfuatilia Lissu ilikuwa na namba batili huku gari halisi yenye namba hizo za usajili ikiwa Arusha.

“Utoaji wa taarifa na wenyewe haukuwa rasmi kwa mfano Lissu aliposema kuna gari inamfuatilia nilielekeza polisi wakaifuatilia ikakutwa Arusha kuna gari ndogo ya namba hizo kwa hiyo kuna moja iliweka namba batili.

“Ile gari ilikutwa kule kule na haikuwa na ruti ya huku (Dar es Salaam) huwa iko kule kule, kwa hiyo kwenye mambo haya ndiyo maana tunahitaji sana ushirikiano.

“Natamani watu hawa tungewatia nguvuni pale pale ningepewa ‘tip’ mapema tungefuatilia hili na  kitendawili cha watu wasiojulikana tungekitegua mara moja,” amesema Mwigulu akihojiwa na Kituo cha Televisheni cha Clouds, leo.


Pamoja na mambo mengine amesema Lissu mwenyewe anaweza kusaidia uchunguzi katika tukio hilo ambapo pia ameonya watu watu wanaotengeneza matukio ya aina hiyo kufikiria madhara yanayoweza kutokea baada ya tukio.
;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;

Waziri wa mambo ya ndani amefanya mahojiano katika kipindi cha Clouds 360 na watangazaji wamemuuliza juu ya matukio yanayofanywa na watu wasiojulikana. 

KUHUSU KUSHAMBULIWA KWA LISU
=> Kuna vitu vingi ambavyo bado tunasita kuvisema hadharani lakini wananchi wawe na imani na kazi ambayo tunaendelea kuifanya na watapewa taarifa.

=> Uchunguzi ulianzia eneo la tukio aliposhambuliwa na kuna taarifa zimeshachukuliwa kutoka maeneo mbalimbali ambazo zinahusiana na tukio hili na zinafanyiwa kazi.

=> Ni tukio linaloudhi na tunahakikisha kwamba tunapata undani wake na kuwapata wanaohusika.

=> Hakuna ukomo wa uchunguzi mpaka pale uchunguzi utakapokamilika na matukio haya ya watu kushambuliwa yameshakuwa mengi tofauti na hili la Lisu.

=> Sio matukio yote yanayohusisha polisi kushambuliwa ndio watuhumiwa hupatikana haraka bali ni utofauti wa mazingira na vifaa vinavyotumika ndivyo vinarahisisha au kukwamisha kwa watuhumiwa kukamatwa kwa haraka.

=> Hatubagui watu kwa itikadi zao wala rangi zao bali ni kila mtanzania bali ni mazingira ya tukio ndiyo yanahusika sana kwenye uchunguzi.

=> Tumeshakamata magari zaidi ya 10 ambayo yanafanana na gari lililofanya tukio. Hatuwezi kusema zaidi kwasababu ni mambo ya ndani sana ya kiuchunguzi na siwezi kuyasema hadharani kutokana na jambo lenyewe kuwa ni nyeti sana mpaka litakapokuwa tayari.

=> Serikali tunaendelea kupata taarifa za maendeleo ya afya yake kupitia balozi lakini mimi binafsi sijaenda.

=> Kwa taratibu zetu kuna watu ambao wanafanya kazi ya kuwasiliana naye pamoja na dereva wake ili kuweza kupata taarifa zinazoweza kusaidia kwenye uchunguzi.

=> Sisi tunatamani sana dereva asaidie kwenye kutoa taarifa sababu tunazani angeweza kutusaidia taarifa nyingi hata magari tuliyakamata tulitegemea yeye atusaidie kuja kuyatambua maana yeye aliliona gari husika.

=> Ila alipoitwa na polisi Dodoma watanzania wengi walilichukuliwa swala hili kwa mtazamo hasi na kudhani kwamba polisi wanataka kumkamata dereva lakini hapana, Nia yetu ni kutaka kushirikiana naye kwenye uchunguzi wa tukio hili.

KULETA WATU KUTOKA NCHI ZA NJE KUFANYA UCHUNGUZI

=> 
Tunashughulika na usalama wa raia wetu pamoja na matukio yanayowadhuru raia wetu.

=> Kazi inayofanywa na jeshi la polisi ni kubwa sana ila tu kwasababu hatuwezi kusema hadharani jinsi kazi inavyofanywa ndio maana wengi hawajui.

=> Sisi kama wizara hatutapenda kuitangazia nchi kwamba jambo la usalama wa nchi na raia kwamba limetushinda. Hii itakuwa jambo la aibu sana kwa nchi hata dunia nzima.

=> Tunataka kila shambulio la umwagaji damu ya mtu yoyote uchunguzi wake uwe mkubwa zaidi kuliko matukio mengine tunayoyafanya kikawaida.

=> Kila kifo kikishatokea au shambulio la kutaka kuua mtu inatakiwa uchunguzi ufanyike wa kina.

=> Mfano kifo cha Mtikila kilijadiliwa sana hivyo halitakiwi kuchukuliwa kama jambo la kawaida, Pia kupotea kwa Ben saanane.

=> Watu wengi ni waoga wa kutoa taarifa za matukio mabaya yanayotokea na hii inaleta ugumu kwenye taasisi yangu kulishughulikia hili.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo