=> Kuna vitu vilionekana kuwa dhahiri lakini baada ya uchunguzi haikuwa hivyo.
=> Tulidhani kijana yule ni polisi lakini baada ya uchunguzi tulibaini kwamba hakuwa polisi. Na kijana yule hakuwa na sare.
=> Hivyo kwakuwa hakuna sare muhalifu pia alikuwa na nafasi ya kutumia nafasi hiyo kufanya uhalifu wake na kwa kuwa hakuwa na sare inakuwa ngumu kumtambua.
=> Suala la ulinzi kwa viongozi yapo kwa mujibu wa sheria lakini kuna baadhi ya wabunge sheria haijawasemea kwamba wawe na walinzi hivyo tunashughulikia hili kwa sasa.
=> Tutaongeza ulinzi kwenye maeneo yote ya viongozi na kufanya doria za mara kwa mara.
=> Baada ya Lisu kusema anatishiwa maisha tuliongeza ulinzi lakini shida ni jinsi alivyokuwa anatoa taarifa hadharani hii ingeweza hata kuwapa mwanya wale waliokuwa wanapanga njama za kumdhuru kujipanga zaidi.
=> Alipotaja gari inayomfwatilia niliagiza gari hiyo itafutwe na suala hilo lilifanyika na watu waliopatikana walihojia lakini gari ikaonekana kuwa tofauti na ile aliyoitaja na gari hiyo ilionekana kwamba haijafanya safari yoyote kwenye maeneo ambayo Mhe Lisu alikuwepo.
