skip to main |
skip to sidebar
Miili iliyokutwa eneo la bahari Coco Beach haijulikani ilikotoka - MAMBOSASA
KAMANDA wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema miili ya wanaume watatu iliyokutwa pembezoni mwa Bahari ya Hindi eneo la Coco Beach hawajui imetoka wapi hivyo wanaendelea na uchunguzi kubaini ilipotoka.
Mambosasa amesema jeshi la polisi linaendelea kupeleleza ili kujua miili hiyo imetokea mkoa upi, nchi gani na wajulikane watu hao ni wakina nani.
“Miili hiyo haieleweki inatoka wapi na watu wenyewe hawajulikani kama wanatoka Tanzania, Msumbiji au Angola hivyo tunaendelea kuichunguza,” amesema Mambosasa.
Maiti za watu ziliokotwa juzi katika eneo hilo mbili zilifungwa kwenye viroba huku nyingine imekutwa na jiwe kubwa lililofungwa na kamba.
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi