Lazaro Nyalandu ameandika ujumbe huo kwenye ukurasa wake wa twitter, na kusema kwamba sasa nchi ya Tanzania inahitaji katiba hiyo ili kuwe na mipaka ya muingiliano wa kazi kwenye mihimili ya nchi.
"Tanzania inahitaji katiba mpya mihimili ya utawala iwekewe mipaka iliyo wazi, na kuwepo 'checks and balance' kwa serikali, bunge, na mahakama", ameandika Lazaro Nyalandu.
Hivi karibuni suala la mchakato wa katiba mpya limekuwa suala ambalo limeonekana kuwekwa kando, kwa kutozungumziwa na viongozi, jambo ambalo limeanza kuzua sintofahamu.
Alichokiandika Lazaro Nyalandu twitter.