Angalia Picha zote za wabunge wa UKAWA Walivyosusa bungeni leo

Wabunge wa CUF na CHADEMA wanaounga mkono UKAWA wakiwa ndani ya mavazi meusi nje ya bunge baada ya kususia kuapishwa wabunge wapya 7 wa CUF.

WABUNGE wa Kambi ya Upinzani Bungeni wamesusia kuapishwa kwa wabunge saba Viti Maalumu wa Chama cha Wananchi (CUF) katika mkutano wa nane Bunge la 11 kwa madai hawakufurahishwa na maamuzi ya kufukuzwa wabunge 8 wa Viti Maalumu wa chama hicho.

Wabunge wa CUF na CHADEMA wanaounga mkono UKAWA wakiwa ndani ya mavazi meusi nje ya bunge baada ya kususia kuapishwa wabunge wapya 7 wa CUF.
Mkutano wa nane wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania umeanza leo Mjini Dodoma na moja ya mambo yaliyopo kwenye ratiba ya mkutano huo ni kuapishwa kwa wabunge 7 wapya kati ya 8 wa Viti Maalumu ambao waliteuliwa kuziba nafasi za wabunge wa Viti Maalumu waliofutwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Prof. Ibrahim Lipumba baada ya kupoteza sifa ya kuwa wabunge.

Wabunge wa CUF na CHADEMA wanaounga mkono UKAWA wakiwa ndani ya mavazi meusi nje ya bunge baada ya kususia kuapishwa wabunge wapya 7 wa CUF.

Wabunge ambao wamekula kiapo cha uaminifu siku ya leo Septemba 5 ni pamoja na  Alfredina Kaigi, Kiza Mayeye, Nuru Bafadhili, Rukia Kassim, Shamsia Mtamba, Sonia Magogo na Zainab Amir.
Wabunge wa CUF na CHADEMA wanaounga mkono UKAWA wakiwa ndani ya mavazi meusi nje ya bunge baada ya kususia kuapishwa wabunge wapya 7 wa CUF.

Aidha, CUF kimewaapisha wabunge saba badala ya nane kama inavyotakiwa kutokana na mbunge mmoja mteule Hindu Mwenda kufariki siku ya Ijumaa Septemba Mosi  katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Kwa upande mwingine, wabunge wa upinzani waliingia bungeni baada ya wabunge hao kumaliza kuapishwa na Spika Job Ndugai.

JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo