Msigwa afunguka Mauaji ya aliyefichua Ujangili wa Meno ya Tembo

Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya (CHADEMA) Mchungaji Peter Msigwa amefunguka na kusema kifo cha Bw Wayne Lotter aliyeuawa usiku wa tarehe 17/08/2017 kwa kupigwa risasi ni pigo kubwa kwa wapambanaji wa ujangili.


Mbunge Peter Msigwa amesema hayo kupitia mtandao wake wa kijamii wa facebook na kusema kifo chake ni cha kusikitisha na hakiwezi kusaulika
"Dunia ya wahifadhi wanyamapori na utalii, wapambanaji wa ujangili na washirika wote tumempoteza mmoja wa manguli wa mapambano dhidi ya ujangili Tanzania Bw Wayne Lotter aliyeuawa usiku wa 17/08/2017 kwa kupigwa risasi karibu ya Shule ya Kimataifa ya Tanganyika IST Masaki jijini Dar es salaam. It's a real shock and an unforgettable loss" alisema Peter Msigwa 
Kwa mujibu wa mtandao wa The Guardian wa nchini Uingereza umeripoti kuwa kiongozi wa taasisi isiyo ya kiserikali ya PAMS Wayne Lotter, 51, alipigwa risasi jijini Dar es Salaam na kusema alikuwa akiendeshwa kutoka uwanja wa ndege akielekea kwenye hotel lakini baadaye gari aliyokuwa amepanda ilisimamishwa na gari jingine ambalo lilikuwa na watu wawili, mmoja akiwa na silaha alifungua mlango aliokuwa ameketi Wayne Lotter na kumpiga risasi
Bw Wayne Lotter ndiye muanzilishi wa PAMS foundation  inayojihusisha na kuzuia unjangili Tanzania, Polisi wanaendelea na uchunguzi kufuatia mauaji hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo