Tume Huru ya Uchaguzi Kenya ilitangaza Kenyatta kuwa mshindi kwa kupata kura 8,203,290 (54.27%) dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga 6,762,224 (44.74%), kufuatia matokeo hayo Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ametoa pongezi kwa Uhuru Kenyatta kwa kuchaguliwa kwa mara nyingine tena.
"Nakupongeza Ndg.Uhuru Kenyatta kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Kenya kwa kipindi kingine. Nakutakia mafanikio mema" alisema Rais Magufuli kupitia mtandao wake wa Twitter
Kwa mujibu wa Tume Huru ya Uchaguzi Kenya (IEBC) ilisema kuwa uchaguzi huo ulikuwa wa huru na haki na kudai kuwa umekuwa ni uchaguzi wa kipekee kwa Kenya kwani watu waliojitokeza kujiandikisha na kupiga kura ni wengi zaidi ukilinganisha na chaguzi zilizofanyika kipindi cha nyuma.
