Serikali imetangaza kukikatia umeme leo hii kiwanda cha Rhino cha
mkoani Tanga kutokana na kudaiwa bili kubwa ya umeme
Akizungumza leo mbele ya Rais John Magufuli, Naibu waziri wa
Nishati na Madini Dkt Medadi Kalemani amesema kiwanda cha Rhino Kitakatiwa
Umeme baada ya shughuli za uzinduzi wa kiwanda cha saruji cha Kilimanjaro ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais la kukata umeme kwa wale wote
wanaodaiwa
Rais Magufuli yupo Mkoani Tanga na hii leo anazindua kiwanda
kikubwa cha Kutengeneza saruji cha Kilimanjaro kilichopo mkoani humo, hivyo
waziri Kalemani amesema kiwanda hicho hakidaiwi bili ya umeme, lakini suala la
kukatikakatika kwa umeme linashughulikiwa mara moja
Bonyeza hapo chini umsikilize:-
Bonyeza hapo chini umsikilize:-