Baadhi ya wafanyabishara wa soko la Sido lililoteketea kwa moto hivi karibuni wakiwa wamebadirisha nyuso zao kutoka kwenye huzuni waliyokuwanayo baada ya kuteketea kwa vibanda vyao vya biashara, Serikali mkoani Mbeya imeridhia wahanga wa moto katika soko la sido kuendelea kubaki katika maeneo yao ya awali na kuagiza wajenge vyumba vya kudumu ili kukabilina na majanga ya moto yanapojitokeza.
Akitoa maelekezo ya serikali mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla amewaagiza watendaji wa halmashauri kupiga kambi katika eneo la soko la Sido haraka kuanzia siku ya kesho kwa ajili ya kubuni michoro na mpangilio wa soko hilo ili wafanyabiashara waanze ujenzi.
Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa wilaya Ya Mbeya Mjini,mkoa ikiwa ni Pamoja na mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini Mh.Joseph Mbilinyi pamija na Naibu spika Bi.Tulia Akson ambaye ametoa msaada wa shilingi milioni 10 kwa wahanga hao.
Aidha baada ya kutolewa kwa kiasi hicho mkutano huo umeridhia fedha hiyo ibaki na mkuu wa mkoa huku uongozi wa soko ukipanga matumizi ya fedha hiyo.
Hata hivyo mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh.Makalla ameliagiza jeshi la zimamoto kuendelea kutoa elimu ya zimamoto,kusambaza vithibiti moto na kuchimba visima vya maji vya ziada katika masoko huku akiwataka viongozi wa ngazi zote za mkoa kuchukua tahadhari za moto kwenye masoko kutokana na ripoti kuonesha chanzo cha janga hilo ni mabaki ya moto uliotokea kwenye moja ya vibanda vya mamalishe waliokuwa ndani ya soko hilo.
Imefahamika kuwa chanzo cha moto ktk soko la SIDO Mbeya ni jiko la mkaa ktk kibanda cha mama lishe na umesababisha hasara ya zaidi ya bil 14 pic.twitter.com/rKyKrEfl3h— MO Dewji Blog (@DewjiBlog) August 23, 2017