Vitendo vya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia vinavyotokea katika wilaya
ya Makete mkoani Njombe havina budi kuendelea kupigwa vita na kila mtu ili
kuwanusuru watoto hasa wa kike
Hayo yamebainika katika kikao cha mwaka cha timu ya Ulinzi wa mtoto
kilichofanyika jana katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Makete
kilichowashirikisha pia wadau mbalimbali wa masuala ya watoto
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho Mkuu wa wilaya ya Makete Mh
Veronica Kessy mbali na kukemea vitendo hivyo lakini pia ameonesha masikitiko
yake baada ya kupokea taarifa za wanafunzi watano wa shule ya sekondari
Kipagalo kupata ujauzito ndani ya mwaka huu
Bonyeza hapo chini Umsikilize:-