Baada ya kupatikana Mtangazaji wa Azam TV dada yake afunguka

Mapema leo kulikuwa na taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Mtangazaji wa Azam TV Fatma Ramole kutojulikana mahali alipo kwa zaidi ya saa 48 na zikatolewa taarifa nyingine leo mchana kuwa amepatikana akiwa Hospitali baada ya kupata ajali maeneo ya Chuo cha Ustawi, Bamaga.

Baada ya taarifa za kupatikana kwake, dada yake anayeitwa Lulu Ramole naye alithibitisha kuwa amepatikana ingawa hakuwa na uwezo wa kuzungumza zaidi akisema taarifa zaidi ziko Polisi.

“Nipo hapa Polisi tunamalizia. Tumeweza kumfuata asanteni tumempata. Siwezi kuongea chochote cha zaidi taarifa zipo Polisi.” – Lulu Ramole.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo