Rais Magufuli afungwe Breki, asema Halima Mdee

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Chadema Halima Mdee kwa mwenendo anao kwenda nao Rais Magufuli analipeleka taifa pabaya na kwamba Watanzania wanapaswa kumfunga breki kwa kuonesha kutofurahishwa na matendo yake.


Mdee ameyasema hayo leo Julai 3, wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika makao makuu ya chama hicho Jijini Dar es salaam, kuhusu kauli ya Marufuku ya mwanafunzi atakayejifungua hatorudi shuleni aliyoitoa Rais Magufuli hivi karibuni.


Mdee ameupinga msimamo huo huku akimtaka rais afuate sheria na katiba ya nchi inayowaruhusu watoto hao warudi shule baada ya kujifungua.

Aidha, Mdee amesema kuwa anashangazwa na Waziri wa Afya, Dkt. Ummy Mwalimu ambaye amesema agizo hilo kuwa lisiendelee kuzungumziwa wakati wanaoumia ni watoto wenyewe ama kwa kubakwa na kusababishiwa ujauzito na hivyo ya Ummy inawanyima haki watoto kuendelea na masomo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo