Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 3 Julai, 2017 amewasili mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongela pamoja na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Mwanza.
Akiwa mkoani hapa Mhe. Rais Magufuli atakuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi wa uboreshaji wa huduma ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Sengerema tarehe 4 Julai, 2017.
Katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza Mhe. Rais Dkt. Magufuli amekutana na kamati ya amani ya viongozi wa dini na kuwashukuru viongozi hao kwa sala na dua zao na amewataka waendelee kuwahimiza waumini wao kuliombea Taifa ili liepukane na vitendo vya rushwa ambavyo ni adui wa maendeleo.
Akiwa njiani kutoka Uwanja wa Ndege wa Mwanza katika eneo la Bwiru kuelekea Ikulu ndogo ya Mwanza, Mhe. Rais Magufuli msafara wake umesimamishwa mara kwa mara na wananchi waliojaa barabarani na kuamua kuzungumza nao ambapo amewahakikishia kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imepania kupambana na ufisadi kwa lengo la kuwaletea maendeleo Watanzania bila kujali tofauti za dini au Siasa.
Aidha, amewahakikishia wananchi hao kuwa Serikali yake imedhamiria kuondoa kero mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufuta baadhi ya kodi zenye kero na kuwapatia vitambulisho wafanyabishara wadogo wadogo, maarufu kama Wamachinga, ili waweze kufanya biashara zao bila kusumbuliwa.
Akiwa eneo la Nyamagana jijini Mwanza, Mheshimiwa Rais alitembea kwa miguu huku kuwasalimu wananchi waliokuwa wakimshangilia na kuzuia msafara wake. Rais Magufuli pia alikwenda Uwanja wa Mpira wa Nyamagana na kuungana na baadhi ya wananchi waliokuwa wakiangalia mechi ya mpira wa miguu kati ya timu ya Buhongwe na Nyamwaga.
Mhe. Rais Dkt. Magufuli pia amefurahishwa na maendeleo ya ujenzi wa barabara ya kutoka Uwanja wa Ndege wa Mwanza hadi katikakati ya jiji ambao gharama za ujenzi wake zilitokana na fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe za Muungano.
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Mwanza
03 Julai 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Viongozi wa Dini mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia ngoma za asili kutoka kikundi cha Bujora mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiombewa sala na Viongozi mbalimbali wa dini kutoka Kanda ya ziwa mara baada ya kuwasili mkoani Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Kona ya bwiru katika barabara ya Airport wakati akitokea uwanja wa ndege wa Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa katikati ya jiji la Mwanza waliokusanyika kumpokea.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akinunua Karanga kutoka kwa Mmachinga anayefanya biashara katikati ya jiji la Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akinunua Karanga kutoka kwa Mmachinga anayefanya biashara katikati ya jiji la Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi wa katikati ya jiji la Mwanza wakati akielekea Uwanja wa Nyamagana kuangalia mechi kati ya Buhongwa United na Timu ya Nyamwaga.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Wachezaji wa Buhongwa Fc mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Nyamagana.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono washabiki wa mpira wa miguu wakati akitoka katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza. PICHA NA IKULU