Mbunge wa Kibamba(Chadema), John Mnyika, amemuuliza Rais wa Jamhuri wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kuwa lini atateua Waziri wa Nishati na Madini.
Mnyika ameuliza swali hilo kupitia ukurasa wake wa Tweeter ambapo ametweet hivi huku akitupia tag kwa Rais Magufuli:
Mheshimiwa Rais @MagufuliJP lini utateua Waziri wa Nishati na Madini?
Mei 24, Rais Magufuli alitengua uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo.