Moja ya kesi zilizokuwa gumzo leo July 17, 2017 katika Mahakama ya wilaya ya Kinondoni ni pamoja na kesi namba 21/2017 ya ubakaji ambayo ilikuwa inamkabili Mganga wa kienyeji Wilson Mkomi mwenye umri wa 30.
Mahakama hiyo imemtia hatiani Mshtakiwa na kumuhukumu kifungo cha miaka 30 jela katika kosa la ubakaji ambalo alilitenda December 29, 2016 maeneo ya Kawe Ukwamani, Kinondoni.
Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu wa Mahakama hiyo Joyce Mushi ambapo alisema mshtakiwa ametiwa hatiani kwa kosa la ubakaji hivyo anahukumiwa kifungo cha miaka 30 jela.