Lissu: Katibu Mkuu wetu, Dkt Vicent Mashinji amepata dhamana ya Polisi

Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa TLS, Tundu Lissu amesema Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo (CHADEMA), Dkt Vicent Mashinji amepata dhamana ya Polisi huku akidai kwamba kiongozi huyo ameambiwa aripoti kesho ambapo lakini hadi sasa hawajajua anatakiwa kuripoti kwa RPC au kwa nani.
Mhe. Lissu ameyaasema hayo leo Dar es Salaam wakati akizungumza na wanahabari na kueleza kuwa baadhi ya viongozi wa Chadema waliokuwa wamekamatwa ni pamoja na mjumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho Waziri Mkuu wa Zamani, Mhe. Edward Lowassa na Mbunge wa Kawe Halima Mdee.
“Muda mfupi uliopita katibu Mkuu wetu, Dkt Vicent Mashinji amepata dhamana ya Polisi huko alikokamatiwa Mbambabay na tumeambiwa kwamba ameambiwa aripoti kesho sasa haieleweki ni kwa RPC au kw Mkuu wa Mkoa au ka mkubwa gani mwingine lakini tumeambiwa anatakiwa aripoti mahali na hivi tunavyozungumza utaratibu unafanywa, kwa taarifa ambazo sina sababu ya kuzitilia shaka utaratibu unafanywa wa kumpeleka Mhe. Edward Ngoyai Lowassa waziri Mkuu mstaafu pamoja na mgombea urais aliyepigiwa kura na na Watanzania Milioni 6 kufikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kosa lile lile ambalo alishtakiwa nalo Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,” amesema Lissu.
“Wengine aidha wamekamatwa au wamefikishwa Mahakamani kwa makosa yanayoendana na hayo uchochezi na vitu kama hivyo kuna wananchama qwetu zaidi ya 51 wa wilaya ya Chatowako mahabusu na kwa Watanzania wengi kwa mamia na kwa maelfu ambao ambao wamekamatwa na kuwekwa mahabusu za polisi na wengine kufikishwa Mahakamani kwa makosa ya kutumia simu zao kwa kutoa maioni yao kwen ye mtandao na kuyaposti mitandaoni , mitandao ya kimawasiliano.”


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo