Taarifa Kwa vyombo vya habari
Mimi Anna mgwira nimejivua uwanachama wangu ACT-Wazalendo ili nikaweze kuwatumikia wana Kilimanjaro
Kwakua nimejivua uwanachama mwenyewe moja Kwa moja nyadhifa zangu zote zitakuwa hazipo
Namshukuru sana mh zitto Zuheri kabwe na wanachama wote ACT-Wazalendo kwakuniamini na kunipa nafasi ya kuwaongoza
Hivyo kuanzia Leo tarehe 4/6/2017 Mimi sio mwanachama tena wa ACT-Wazalendo
Kazi yangu sasa ni kuwatumikia wananchi kupitia nafasi yangu ya sasa ya Ukuu wa Mkoa Kilimanjaro
Hii ni heshma kubwa kwangu na Kwa familia yangu Kwa ujumla
Mungu awabariki
Anna mgwira
Leo 4/6/2017: saa7:30 mchana
Hata muda mchache baada ya kusambaa kwa taarifa hiyo, Ofisa habari wa chama cha ACT-Wazalendo Abdallah Hamisi amekanusha taarifa hiyo.