KATIBU Mkuu wa Chama Cha Wananchi Maalimu Seif Sharif Ahamad amesema kuwa Rais Magufuli amefanya jambo la kihistoria nchini kwa kufanya uteuzi wa watendaji wake kutoka kwenye upinzani.
Maalimu Seif amesema Hayo leo wakati wa Ufunguzi wa Ofisi ya wabunge wa CUF iliyokuwepo Magomeni jijini Dar es Salaam.
"Ana Mamlaka kikatiba kumteua yoyote,"
amesema kuwa jambo hilo sio geni kwenye nchi zilizoendelea kama vile Ulaya na Amerika ambapo Hata Rais Mstaafu wa US Barack Obama aliwahi kufanya hivyo.