Serikali yatoa ufafanuzi kung'olewa Kibao cha mtaa wa Victor Wanyama

Baada ya taarifa za mchezaji wa Tottenham, Vicent Wanyama kupokwa mtaa uliopewa jina lake hatimae Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Ubungo NHC, Amani Sizya amefunguka sababu za kufutwa kwa mtaa huo.

Akifunguka sababu za kufutwa kwa mtaa huo Bw. Sizya amesema ni kutokana na kutofuata taratibu wakati wa kutangazwa kwa mtaa huo.
Kila jambo linautaratibu wake hata ukitaka kubadilisha jina la barabara lazima ufuate utaratibu kwahiyo hakukuwa na utaratibu uliofuatwa unajua ilikuwa haraka sana, lakini niseme tuu kwamba hili litafanikiwa na mtaa huo utatumika kwa jina hilo wakifuata taratibu,“amesema Sizya.
Victor Wanyama wiki iliyopita alipewa mtaa ujulikanao kama Viwandani eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam ili rasmi uanze kutambulika kwa jina lake lakini jana Serikali ya mtaa huo iling’oa kibao cha maelekezo na kufuta mtaa huo.
By Godfrey Mgallah


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo