Mwalimu ajiua akiwa gesti, aacha ujumbe mzito


Sumbawanga. Mwalimu, Betson Sanga  aliyekuwa akifundisha Shule ya Sekondari Milundikwa iliyopo wilayani Nkasi mkoani Rukwa amefariki dunia baada ya kunywa sumu akiwa katika nyumba ya kulala wageni mjini hapa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando amesema kwamba mwalimu huyo alifariki dunia juzi usiku huku akiwa ndani ya chumba alichokuwa amepanga katika nyumba moja ya kulala wageni iliyopo eneo la stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani.

Kyando amesema chanzo cha kifo cha mwalimu huyo bado hakijafahamika lakini aliacha ujumbe mfupi wa maneno.

“Kama anadaiwa deni lolote na mtu amweleze mkurugenzi ambaye ni mwajiri wake, lakini asilaumiwe chochote juu ya kifo chake," amesema Kamanda Kyando wakati akinukuu ujumbe huo wa marehemu.

Kamanda Kyando pia amesema uchunguzi wa kitabibu umebainisha kuwa mwalimu huyo alijiua kwa kunywa sumu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo