Rais awaita wapinzani kwenye mkutano wake huko Pwani


Rais John Magufuli ametumia mkutano wake wa kwanza mkoani Pwani kuwataka viongozi wa upinzani ambao wamepokea mwanachama mpya kutoka CCM kutumia mkutano huo kuwatangaza.

Rais alitoa fursa hiyo mara mbili leo (Jumanne) katika mkutano wake wa hadhara  wakati mwanachama wa ACT-Wazalendo aliyehamia CCM alipotambulishwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole.

“Kama kuna mwana CCM amehamia Chadema, aje hapa atangaze, namkaribisha, nipo hapa kuzindua viwanda sijaja kichama lakini nimpishe, nikae pembeni nimuache Katibu wa Uenezi amkaribishe mwana CCM mpya,” amesema.

Hata baada ya mwanachama huyo mpya kutambulishwa na kupata nafasi ya kutoa neno, Rais aliporudi jukwaani na zungumza tena alisema kama wapo viongozi wa Chadema au CUF wamepata mwanachama wa CCM aliyehamia katika vyama vyao, wanaruhusiwa kumtangaza katika mkutano huo.

“Hata kama ni wa CCM amehamia CUF aje atangaze na kama CUF kahamia Chadema, nao pia waje wamtangaze hapa,” amesema.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo