Mazingira yaendelea Kutunzwa Butiama, Majiko ya Kisasa Yasambazwa

Na Asha Shaban, Mara

Kutokana uchafuzi wa mazingira na ukataji wa miti kwa ajili ya matumizi ya misitu na kuni Shirika lisilo la kiserikali global ressource Alliance Tanzania kwakushirikiana na mradi wa gosol  kutoka begonia Finland wamezindua maradi Wa majiko ya mionzi ya jua (solar) nchini Tanzania katika wilaya ya Butiama mkoani Mara.


Jiko Hili la mionzi ya jua limetengenezwa maalumu kwa Ajili ya viwanda vidogo vidogo na Makundi ya akina mama wajasilia mali ambao wanafanya shughuli za uokaji kama mikate na vyakula mbalimbali.

Akiongea wakati wa uzinduzi huo meneja uendeshaji Heikki lindfors alisema kuwa majiko haya yanakuja kupunguza matumizi ya mkaa na kupunguza hewa ya okaa

Alisema kuwa miti tani 9.5 hukatwa kilamwakwa duniani kote na watu zaidi ya bilion 3 wanatumia mkaa duniani.

Sambamba na hilo ameongeza kuwa majiko haya yanatumika hata nchi za Baridi na wameweza kutumia teknolojia hii Kwenye nchi ambayo haikuwa na umeme wala mkaa  nakutolea mfano nchi ambazo zimeisha tumia teknolojia hii na kufanya vizier kama kenya ,India ,Nigeria pamoja na us

Bi. Monica macha ni mjumbe toka kikundi cha alfa women group wameshukuru kwaekupatiwa jiko hili la mionzi ambapo amesema watalitumia katika kazi zao za ujasiliamali kwa kuokea mikate na vyakula vingine.

Macha alisema kuwa was katika kikundi chao kila moja wao analea mtoto mwenye mazingira magumu hivyo kupata jiko hilo litawasaidia kupata pesa kwa urahisi na kuwaudumia watoto hao na kupanua bishara yao

Kwa upande wake kaimu mkurugenzi mtendaji wa global resource alliance madaraka nyerere alisema kwakuwa mashirika haya yameona umuhimu wa kutunza mazingira basi anaiomba serikali kutoa msaada kwa mashirika kama hayo Kwa kuondoa ushuru katika malighafi zinazo tumika katika matengenezo ya majiko hayo

"naishukuru serikali kwa kuamua kumuenzi Hayati mwl.julius Nyerere kwa kuwa alikuwa ni mtu wa mzingira "alisema.

Ameongeza kuwa  shirika la global resource alliance ndio wenyeji wa gosol hapa tanzania na wao ndio wanaoratibu vikundi ambavyo vitapatiwa majiko hanayo tumia nishati yadidifu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo