Mtu mmoja aliyefahamika kwa majina ya Nuhu Mgeta (35) mkazi wa kijiji cha Kisabo wilayani Magu mkoani Mwanza anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma ya mauaji ya mtoto wake wa kiume Misungwi Nuhu (6) baada ya kumziba pua kisha kumtupia kwenye dimbwi la maji.
Imeelezwa kuwa mtuhumiwa alikuwa akiishi na watoto wake kutokana na kutengana na mke wake kwa muda mrefu.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa baada ya upelelezi kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.
Baadhi ya wananchi wamelaani tukio hilo na kuliomba Jeshi la Polisi kumchukulia hatua kali za kisheria mtu huyo.