Kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Ramadhani Nombo mkazi wa Dar, amekamatwa leo Juni 19, 2017 akijaribu kuingiza simu 5 katika Gereza la Mahabusu la Keko.
Kijana huyo alikuwa amezifunga simu hizo kwenye mapande ya nyama yaliyorostiwa kama inavyoonesha kwenye picha. Simu hizo zilikuwa ziingizwe gerezani humo ili wapewe wafungwa kwa ajili ya mawasiliano jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Kamanda wa Magereza wa Mkoa wa Dar, DCP Mboje ambaye amethibitisha kukamatwa kwa kijana na kusema kuwa amepelekwa polisi ili achukuliwe hatua za kisheria.